tupendane

Utamutamu


Wimbo mpya wa kijana chipkizi toka iringa huu hapa chiniPakua hapa ni kijana anaye jitahid kufika pazuri muone na muunge mkono

Ugonjwa wa kuwashwa au kujikuna ujulikanao kama burudani


Habari watanzania  ningependa mtambue kuhudu ugonjwa ujulikanao kama burudani ugonjwa huu upatikana sana maeneo ya adhabu yaan maeneo kama mahabusu ama mahakani palee kifungoni ugonjwaa huu ni ugonjea ambao dalili zake ni kama zifatazo

. kuwashwa mwili mzima
.kuhisi homa ama mwili kua wa moto  sana
.mdomo kuungua pembezoni na kuweka kidonda
. kuwashwa sehemu za siri
. kuwashwa matakoni na kuleta uvimbe wa kawaida na mwingine kua mkubwa
. mkononi kua na upele unaowasha sana na kutoa maji maji kama usaa
.miguuni napo kutoa upele wnye kutoa usaa pia ki ujumla naweza kusema hutoa usaa mwili mzima hivo kupelekea kujikuna mara kwa mara tena bila mpangilio na uhumia sana asa sehemu za siri na kwenye mahungio ya mapajaa hujaa vidondaa sana uhumia sana hasa pale unapo rnda kuoga ama kugusana na maji.

 DALILI ZA UGONJWA HUU
. dalili kuu ya ugonjwaa huu ni kujiwasha
. kua na vipele vinavotoa usaa au majimaji
Kujikunaa sehemu za siri pamoja na matakoni

        TIBA KUU YA UGONJWA WA BURUDANI

tiba ya ugonjwa huu ni sindano peke yake hakuna kidonge wala dawa ya kujipaka ila njia ya pekee ya kupona ni kufungwa sindano kutokana na masmbukizi haya kungia kwenye damu moja kwa moja hivo usidanganywe

 Nashkuru sana kwa kusoma mambo haya

Simba sio watu wazuri mpaka mo derwij kaona


Ni baada ya mdhamini wao mkuu wa timu hiyo mr mo dewji kuona uzembe wao hivo kaamua kuwaimiza kufanya madhambulizi au kazi kwa kujituma na sio kubweteka na kungoja maripo ya bure bure hivo amedai wale wachezaji wote ambao mikataba yao inaisha mwaka huu hawata endelea nao mpaka pale watakapo kua wame jilekebisha ka kujutuma


Viongozi 900 tumbo joto, ndani ya siku 31 za uhakiki wa mali zao


Viongozi 900 tumbo joto, ndani ya siku 31 za uhakiki wa mali zao
Leo Juni 11, 2018 Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela amesema tayari wamechagua viongozi 900 kwa ajili ya kuanza kufanya uhakiki wa mali za viongozi hao ili kuthibitisha thamani na uhalisia wa mali hizo na kutambua namna walivyozipata.
Amesema kuwa zoezi hlo linatarajiwa kufanyika ndani ya mwezi mmoja kuanzia Juni 18 hadi Julai 18 mwaka huu.
Aidha uhakiki huo unatarajiwa kufanyika kwa baadhi ya viongozi na si viongozi wote Nsekela amesema ni kutokana na Serikali kutokuwa na fedha za kutosha za kuhakiki viongozi wengi kwa wakati mmoja.
“Sasa tumefikia mahali ambapo tuende kuhakiki kwa baadhi ya viongozi nasema kwa baadhi ya viongozi kwasababu kuna sababu nyingi, sababu kubwa tunasema ni rasilimali fedha tunasema kwamba kama fedha hatuna za kutosha hatuwezi kuwahakiki viongozi wengi kwa hivi sasa tumefanya uchambuzi wa viongozi 900 ambao sasa tunakwenda kuwahakiki” Amesema Nsekela.

Serikali yaburuzwa mahakamani


Fundi Seremala mmoja nchini Kenya ameishtaki serikali akidai kutaka kulipwa $2m (£1.5m) malipo ya viti viwili alivyomtengenezea rais mstaafu Daniel Arap Moi miaka 26 iliyopita.
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Nairobi News’ nchini humo, Solomon Njoroge Kiore amesema kuwa aliwasilisha viti hivyo kwenye ofisi ya maonyesho ya kilimo ya Nairobi kwa hafla ya rais ya siku tatu.
Aidha, Mtandao huo wa habari umeripoti kuwa mawakili wa serikali walidai mwezi Februari kwamba waliafikiana kumaliza kesi hiyo nje ya mahakama lakini hawajawasiliana tena na Kiore tangu wakati huo.
“Rais Mstaafu, Daniel Moi alivitumia viti hivyo kwa mwaka mmoja, kabla ya viti hivyo kurudishwa kwangu”, amesema Kiore
Hata hivyo, Kiore ameongeza kuwa angependelea viti hivyo kuwekwa katika jumba jipya la makumbusho lililopo katika Ikulu ya rais.

Tazama Diamond akifunga ndoa na Zari ndani ya ‘Iyena’


Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini, Diamond Platinumz ameachia ngoma yake mpya inayoenda kwa jina la ‘Iyena’ aliyomshirikisha msanii wake Rayvany.
Ambapo katika video ya wimbo huo aliyekuwa mpenzi wake Zarina Hassan ameonekana akifunga ndoa na Diamond.
Aidha, katika siku za nyuma kwenye mahojiano mbalimbali Diamond Platinumz amewahi kuzungumza juu ya wimbo huo ambapo alisikika akijinadi kuwa tayari ametengeneza wimbo mzuri utakaovuma na kutumika katika maharusi mbalimbali.
Natumaini ndoto yake imetimia kama ilivyo kwa msanii huyo kutokosea hasa pale anapofanya kazi zake, wimbo ni mzuri unachangamsha na utafaa kupigwa katika maharusi mbalimbali.
Aidha uwepo wa Zarina Hassan katika video hiyo unaweza kuleta mtafaruko juu ya mahusiano ya wawili hao ambao walibwagana miezi mitatu iliyopita.
Hata hivyo siku chache zilizopita yalizuka maneno yakidai kuwa Diamond alimpigia magoti Zari kumuomba msamaha ili warudishe penzi lao ila Diamond alipinga tetesi hizo na kudai kuwa alikwenda nchini Afrika Kusini kuwasilimia watoto wake na kuwa yeye na Zari watabaki kuwa wazazi na si vinginevyo.
Bonyeza kitufe chekundu hapa chini kuutazama wimbo wa Iyena.

https://youtu.be/gNXTu6T20n8

Video: Nchi zilizovunja rekodi kuchukua kombe la dunia mara nyingi zaidi


Kuelekea michuano ya kombe la Dunia ambayo mwaka huu inatarajiwa kufanyika nchini Urusi kuanzia June 14, katika kipindi cha Zaidi kimeweza kufanya tafiti mbalimbali juu ya makombe ya dunia yaliyowahi kufanyika miaka ya nyuma.
Katika tafiti hizo kuna rekodi mbalimbali zilizovunjwa na baadhi ya nchi ambapo kuna nchi zimeweza kuchukua kombe hilo zaidi ya mara tano.
Aidha mara nyingi imekuwa ikitokea nchi inayokuwa wenyeji wa michuano ya kombe la dunia huwa na asilimia kubwa ya kuchukua kombe hilo, Je mwaka huu Urusi itatwaa kombe hilo?.
Bonyeza kitufe chekundu kutazama rekodi mbalimbali za nchi zilizowahi kuchukua kombe la dunia mara nyingi zaidi.