makampuni ya ulinzi tanzania yawa gumzo
ZIFAHAMU KAMPUNI ZA ULIZI TANZANIA NA MATATIZO YAKE
zifuatazo ni kampuni za ulinzi zilizopo hapa nchi ambazo ni kubwa ukilinganisha na nyingine
G4S
SGA
KKK
CHUI
ALTIMATE
NIGHTSUPORT
hizo ni kwa zile kubwa kubwa ila zipo nyingi zaidi ya campuni 128 tanzania nzima
ZIFUATAZO NI KERO ZIWAPAZO WALINZI WA TANZANIA SECURITY
1/HUKOSAJI WA VITENDEA KAZI,kwa hapa tunazungumzia vitendea kazi kama silaha za kujihami wawapo lindoni mfano rungu,radio call,bunduki,hata ata silaha za jadi km mishale na upinde kwahiyo katika hili walinzi wengi wamekua wakiuza uhai wao kwa kile wakiitacho kutafta liziki vilevile wamekua wakikosa kujiami kutokana na kukosa vifaa hivo japo baadhi ya malindo yao yamekua na ulinzi wa mbwa wakari wanao milikiwa na makampuni hayo lakini nayo hiyo njia haijaonekana kuwasaidia walinzi hawa kwasababu si malindo yote yanakua na askari wa mbwa
2/KUDHALAULIWA NA JAMII INAYO WAZUNGUKA,walinzi wetu pia hudharauliwa sana kutokana na kufanya kazi hiyo lakini hii hutokana na mfumo wa kazi hii ulojengeka toka zamani ya kwamba kazi hizi hufanywa na wazee waliokosa uelekeo na kusubiri kujifia hivo basi ukionekana kijana wafanya kazi hii basi hudharauliwa sana na sababu nyingine huletwa na waajili wao pamoja na viongozi wao yaani supervisors ambao uwafokea askari hao hata mbele za watu nayo upelekea kudharauliwa, dharau nyingine uletwa na uongozi dhaifu wa kampuni husika hii uletwa na kampuni baadhi kushindwa kusimamia wavazi ya askari wao ambapoo hushindwa kuwagawia jezi mpya kwa wakati hivo kupelekea kuvaa ovyo ovyonguo zilizo chakaa
4/UKOSA WAPI WAPELEKE VILIO VYAO HASA WANAPO ONEWA
hili ni tatizo pia ambapo security wengi huonewa sana na kukosa wapi wapeleke vilio vyao hiyo uletwa na viongozi wao kuwaonea na kuwaonya kwamba endapo ukamshitaki popote atakufanya kupoteza kibarua hivo humfanya mlinzi kukaa kimya tatizo lingine huja kwa wateja wao wanao walinda ambapo mteja huyo huweza kutunga sheria yoyote anaoyo jisikia kuianzisha kwa sikari hao bila kujali madhara yake ama faida yake sheria nyingi za wateja hasa wahindi wamekua gumzo kubwa kwa walinzi hawa mfano mteja uweza kusema sitaki mlinzi yeyote kutumia choo hichi ama sitaki mlinzi atumie maji ya kunywa hapa hayo ni baadhi ya matukio yawapatao na endapo walinzi wakasema tatizo hilo katika kampuni hao huishia kuambiwa pigeni kazi hii onesha dhaili kwamba makampuni mengi yapo kwa ajili ya pesa na sio kwa usalama wa wafanya kazi wao
5/SERIKARI KUTO ONESHA USHILIKIANO NA RAIA WAO HASA HAWA WALINZI
Serikali yatakiwa kumlika vilio vya wananchi wake katika idala zote na hasa wawekezaji waingiao nchini humu mfano mlinzi wa tanzania hajarusiwa kumkamata mwalifu na kumfikisha kituo cha polisi bali wamukamatapo mwalifu humpeleka kwa mteja wake pia mteja ndo utoa ruhusa na ruhusa hiyo uenda ikawa kwamaba mwalifu aitiwe polisi ama mwalifu asamaehewe kwa kua ni mfanyakazi wake wa maana hivo asipewe adhabu yoyote na kwa kua mteja anakua ndo msemaji wa mwisho upelekea askari kukubali agizo hiulo na kumfanya mwalifu kuendelea kuishi salama katika jamii hiyo serikari pia hukosa kupanga kima cha chini katika makampuni hayo ambayo hupelekea makampuni kutofautiana mshahara ijapo kua utendaji wa kazi yenyewe kua moja kutoka kampuni moja kwenda nyingine
6/UKAGUZI AFIFU WA SERIKARI
ukaguzi katika makampuni haya serikari imekua haikagui mfano unakuta kampuni ya ulinzi imeajiri watanzania 1000000 lakini ukienda makao makuu ya kampuni hiyo unakuta wafanyakazi wote wanaofika hapo wana tumia vyoo vitatu bila kijali huyu ni mwanamke hatakiwi kutumia choo moja na mwanaume .chanagamoto nyigine ni kampuni kukosa japo hosipitali za kuwatibu asikari wao wapatapo matatizo malindoni kwao kama kuvamiwa na kupigwa na kuumizwa hivyo upelekea askari kujitibu mwenyewe kwa kipato chake hicho hicho kidgo bila kuchangiwa na kampuni japo asirimia moja hii uwafanya watanzania wengi kuumia katika kazi hii na kuhisi hawana maana ya kuishi katika nchi yao
7/KUDHARAULIWA NA KUONEWA PALE WANAPOKUA WAMEIBIWA MALINDONI KWAO
Hapa mlinzi huonekana hana maana na hapa usukumizwa polisi na kupigwa sana akilazimishwa aseme kwanini kaibiwa na kuambiwa ameshiriki katika wizi huo kumbe unakuta sio kweri hii imekua tofauti sana nikilinganisha kwamba kazi hii imefanana sana na kazi ya polisi wetu lakini cha ajabu polisi anapo ibiwa kwanini hwezi kuonewa kama waonewavyo hawa wenzetu hawa walinzi serikali hapa iweke usawa
MENGINEYO KATIKA MAKALA HII.,
Pamoja na hayo yalio orodheshwa hapo juu ni madhaifu ya selikari na waanzilishi wa makampuni hayo lakini pia lipo kampuni moja ambalo limeonekana kua bora kuliko mengine hapa nchini ambalo kinajulikana kwa jina la G4S kampuni hii imekua bora kuliko zote kuanzia uvaaji wake unadhifu wa uniform zake na uongozi wake kiujimla pamoja na hayo matatizo hayawezi kukosa mfano kampuni hii inakumbwa na ukosefu wa hospitali za wakuwatibu wafanya kazi wake wapatapo majanga kazini
lakini mengine ni moja ya kampuni ya kuigwa tanzania
kwa mawasiliano kuhusu makala hii na nyingine zijazo tupigie kwa maoni na ushauri kwa namba 067641187
ama temelea blog yetu eddymimi.blogsport.com kwa habari zaidi

0 Comments:
Post a Comment