Hamisa amtaka Diamond kuifunda familia yake..’waambie waheshimu damu yako’
Mapema leo hii mwanamitindo maarufu nchini aliyezaa na Diamond
Platinumz, Hamisa Mobetto amefunguka na kumtaka msanii huyo kuongea na
familia yake juu ya mambo yanayoendelea mtandaoni akionesha hapendezwi
na maneno yanayoongelewa na ndugu wa karibu Diamond juu yake.Mvurugano huu ni kufuatia ujio wa nyimbo ya Iyena ambao umeibua mambo mengi yaliyofichika ndani ya familia ya msanii huyo mkubwa nchini na nje ya nchi Diamond Platinumz.
Ambapo kupitia mtandao wa Instagram Hamisa amefunguka mazito na kufikia kuandika hayo.
”Na tena saa ingine na kaa kimya kuwasitiri kwa mengi na pia @deedylan akikua asione hii migogoro lakini ndugu zako hawabebeki its too much talk to your familia maana wewe ni mwanaume na unauwezo wa kuyamaliza, Na pia waambie unahitaji mke na sio house girl wa nyumba, mwanamke kazi yake kukupikia ule au nilikua sikupikii tena sio wewe tu ndugu zako mkala na kusaza, leo imekuwa Hamisa hajui kupika, kusafisha nyumba kwahiyo chumba chako tukimaliza lalana huwa anasafisha nani? au walitaka niende kuwafulia vyupi vyao nikimaliza niwapigie deki mpaka chumbani kwao? wakishindwa kuniheshimu basi waambie waheshimu damu yako” amemalizia hivyo.
-
Hamisa aibariki ndoa ya Diamond na Zari
Hata hivyo siku za nyuma mama mzazi wa Diamond Platinumz, Bi Sandra amewahi kuhojiwa na moja ya chombo cha habari hapa nchini alisikika akisema siku ambayo mwanaye atafunga ndoa na Hamissa hatohudhuria ndoa hiyo kwa madai kuwa mwanamitindo huyo si mwanamke wa kuoa na kuweka ndani kama mke.
0 Comments:
Post a Comment